Kwa mujibu wa shirika Shirika la Habari la Hawza, Katika hotuba ya ufunguzi wa semina hiyo, Dkt Taqavi, mkurugezi wa Almustafa Tawi la Daresalam Tanzania, aliweka wazi malengo na misingi iliyokusudiwa kuafikiwa. Alisisitiza kuwa; tuna hazina kubwa ya rasilimali watu, maarifa na uzoefu, na kwamba kuna ulazima wa kupanga mikakati madhubuti ili kutimiza malengo hayo.
Alisema kuwa kuna ulazima wa kufuata hatua kama vile: Utumiaji sahihi wa rasilimali na uwezo uliopo katika shule ili kuongeza ufanisi katika utendaji, kuratibu na kusahihisha wa taarifa za kielimu, madrasa kama msingi wa mipango na uamuzi wa kimkakati, na kutathmini changamoto zinazotokana na malezi na mafunzo, ikiwa ni pamoja na kubainisha maeneo yanayohitaji kuboreshwa bila kuchelewa.
Mbali na malengo hayo, washiriki katika semina hiyo walijadiliana kwa kina kuhusiana na fursa zilizo wazi katika sekta ya elimu, ikiwemo uwepo wa nguvu kazi yenye uwezo, mazingira ya kiraia yanayoruhusu ushirikiano wa kikanda, pamoja na uhitaji wa mifumo ya kisasa ya ufundishaji. Vilevile, changamoto kama ukosefu wa vifaa vya kisasa, tofauti za kimtaala, na mahitaji ya uwezeshaji kwa walimu zilijadiliwa kwa mtazamo wa kutafuta suluhu.
Hujjatul-Islam Taqavi alisisitiza umuhimu wa mikakati ya muda mrefu inayojikita katika kuboresha uwezo wa walimu, kutengeneza mazingira jumuishi ya kujifunza, na kukidhi mahitaji ya kimataifa katika elimu.
Sehemu ya mwisho ya semina hiyo ilitumiwa na wakuu wa vituo mbali mbali kuwasilisha maoni, mitazamo na uzoefu wao katika kusimamia taasisi za elimu na utamaduni. Walijadili mbinu za malezi, njia za kuboresha usimamizi, pamoja na umuhimu wa kuwa na miongozo ya pamoja katika kuendesha shughuli zao.





Maoni yako